Skip to main content

UNHCR yaonya wavukao bahari kwenda Yemen

UNHCR yaonya wavukao bahari kwenda Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema licha ya kudorora kwa hali ya kibinadamu itokanayo na mapigano huko Yemen, bado watu zaidi ya 100,000 walivuka ghuba ya Aden mwaka huu kutoka pembe ya Afrika kuelekea nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi, msemaji wa UNHCR William Spendler amesema kitendo hicho ni kinasisitizia umuhimu wa kutoa usaidizi wa kutosha nchi wanazotoka wakimbizi hao, sanjari na vituo vya kati ili kukatisha mipango yao ya kuvuka bahari.

Wasaka hifadhi wanasema heri kukumbwa na magumu njiani kuliko umaskini na mateso katika nchi zao, hivyo Bwana Spindler amesema..

(Sauti ya Spindler)

“Kutokana na hali hii, mwezi wa Disemba, UNHCR inalenga kuzindua kampeni ya kikanda ya kuhabarisha kule maeneo wanakotoka na vituo vya mpito ikiwemo Ethiopia na Somali hao ili kuwaonya juu ya hatari za kuvuka bahari na watakazokumbana nazo Yemen.”