Ajali ya barabarani hukwamisha uwezo wa manusura wa ajali

28 Novemba 2016

Ripoti ya hali ya usalama barabarani ya mwaka 2015 ikiangazia mataifa 180 inasema kwamba idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani imeongezela huku maafa mengi yakishuhudiwa nchi za kipato cha chini.

Kutokana na hali hiyo, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mataifa yalipanga sheria angalau moja kuambatana na sheria za barabarani ikiwemo: kufunga mkanda, dereva kutotumia mihadarati na kuzingatia mwendo kasi.

Licha ya kwamba hatua zimepigwa bado kasi ni ndogo na Umoja wa Mataifa unataka hatua zaidi ili kupunguza vifo vya ajali barabarani kufikia 2020. Nchini Uganda mwandishi wetu john Kibego amezungumza na manusura wa ajali ya barabani ambaye alinusurika kifo lakini kuachwa na majeraha ya kisaikolojia, kama anavyosimulia katika makala hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter