Ban amteua Olufemi kuwa msajili MICT

28 Novemba 2016

Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Olufemi Elias wa Nigeria kuwa msajili wa mfumo uliorithi mahakama za kimataifa za uhalifu nchini Rwanda na Yugoslavia, MICT.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akisema kuwa Bwana Elias anachukua nafasi hiyo kuanzia tareha Mosi mwezi Januari mwakani kufuatia msajili wa awali John Hocking wa Australia kumaliza muda wake.

Ban amemshukuru Hocking kwa utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo kuanzisha mfumo wa MICT huko Arusha ambao unasongesha majukumu ya ICTR ya Rwanda.

Kabla ya uteuzi wa leo, Bwana Elias amekuwa Katibu Mtendaji wa mahakama ya kiutawala ya Benki ya Dunia tangu mwezi Julai mwaka 2016, nafasi ambayo alishikilia pia tangu mwaka 2008 hadi 2013.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter