Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na wasichana wapaza sauti kupitia VOICES ya UNFPA

Wanawake na wasichana wapaza sauti kupitia VOICES ya UNFPA

Wakati siku 16 za kupinga ukatili dhdi ya wanawake zikiendelea kuangaziwa duniani hadi tarehe 10 mwezi ujao, msichana mmoja kutoka Ethiopia ambaye alikumbwa na mila potofu ya ukeketaji amesema ataendelea kuelimisha jamii ili ziepushe watoto wao dhidi ya janga hilo.Taarifa kamili na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Katika chapisho la shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA linalopaza sauti za wasichana na wanawake waliokumbwa na aina mbali mbali za ukatili, Fatuma amesema sasa yeye ni mtetezi katika jamii yake kupitia mradi wa shirika hilo.

Naye Cecilia ambaye alikimbia kutoka Sudan kusini na wanae watatu kutokana na mapigano anasema hivi sasa kupitia mradi wa UNFPA wanasaidia wanawke kujenga stadi za kujikwamua kiuchumi, kujiamini na kuwakwamua wanawake waliokumbwa na ukatili.

Kutoka Uganda, Mary Goret Aleper mwenye umri wa miaka 10 kupitia jarida hilo la VOICES la UNFPA anasema anataka usawa wa kijinsia na ndoto yake ni kuona wasichana watapata thamani kama wavulana.