Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala kuhusu SDG's wabaini mambo Tanzania

Mjadala kuhusu SDG's wabaini mambo Tanzania

Umoja wa Mataifa ikishirikiana na Umoja wa Ulaya umeweza kuwafikia vijana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kuwaelimisha kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDG's na vile vile kusikia kile ambacho kinawatatiza.

Ushirikiano huo umeweza kuwahamasisha vijana katika maeneo ya Arusha, Dodoma, Zanzibar, Kigoma, Mwanza na Simiyu na harakati hizo bado zinaendelea.

Akihojiwa na idhaa hii, mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ambaye ni mmoja wa waendesha semina hizo.. .

(Sauti ya Alvaro)

Halikadhalika Bwana Alvaro amesema katika mijadala hiyo hususan mkoani Kigoma, wenyeji wamelalama vile ambavyo Umoja wa Mataifa unahudumia zaidi wakimbizi na kusahau wananchi walio kwenye mazingira magumu.