Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulimwengu umewasahau watu masikini wa CAR-OCHA

Ulimwengu umewasahau watu masikini wa CAR-OCHA

 Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, moja ya nchi masikini sana, imesahaulika na kutelekezwa, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo Fabrizio Hochschild amesema nusu ya idadi ya watu CAR wanahitaji misaada ya kibinadamu, na hii ni kwa sababu ya vita vya muongo mzima vinavyoendelea na utawala duni, akiongeza...

(Sauti ya Fabrizio)

"Ni mahali ambako mtoto mmoja kati ya watano hawataishi kwa miaka mitano, ni mahali ambako wanawake kumi watakaojifungua, mmoja atafariki dunia, ni mahali ambako takriban nusu ya watoto watakupata unyafuzi utakaoathiri afya zao baadaye".

Kwa mantiki hiyo amesema, dola milioni 400 zinahitajika haraka kusaidia watu zaidi ya milioni moja na nusu ambao kati yao hao , milioni moja ni wale wanaorejea makwao baada ya kukimbia vita.