Skip to main content

Wakazi wa Luhanga DRC waanza maombolezo ya siku nne

Wakazi wa Luhanga DRC waanza maombolezo ya siku nne

Huko jimbo la Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC siku nne za maombolezo zimeanza kuzingatia hii leo kufuatia mauaji ya watu zaidi ya 20 siku ya Jumapili. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Mauaji hayo katika kijiji cha Luhanga yametokana na mashambulizi yaliyofanywa na kikundi cha Mayi-Mayi Mazembe.

Hii leo wawakilishi wa majimbo la Rutshuru na Masisi wameuomba ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO usaidie viongozi hao kwenda Luhanga kushiriki mazishi huku wananchi wakiomboleza kwa mujibu wa mila na desturi.

Kwa mujibu wa MONUSCO waliouawa ni watu 25 ilihali majeruhi 15 walisafirishwa hadi kituo cha matibabu cha ujumbe huo huko Goma kwa ajili ya matibabu.

MONUSCO imelaani vikali shambulio hilo dhidi ya raia, huku ikituma salamu za rambirambi kwa wafiwa, ikisisitiza azma yake ya kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda raia.