Usafiri endelevu ni njia mojawapo ya kufanikisha ajenda 2030

26 Novemba 2016

Katibu mkuu wa Umoja Ban Ki-moon amesema ni wazi suala la umuhimu wa usafiri endelevu halina mjadala.

Amesema hayo leo akifungua mkutaono wa kimataifa wa usafirishaji endelevu huko Ashgabat, Turkmentistan akitaja biashara ya kimataifa kote duniani kuwa inategemea njia tofauti za usafiri iwe ni barabara, reli, majini na njia za anga.

Ban amesema ingawa sekta hiyo ni chanzo kikubwa cha ajira na injini ya ukuaji wa uchumi, bado usafirishaji endelevu haujafikia jamii nyingi zaidi vijijini, mamilioni ya watu wenye ulemavu hawawezi kutumia usafiri wa umma kwa urahisi, sanjari na wazee, wanawake na wasichana.

(Sauti ya Ban)

Usafirishaji endelevu unaweza kusaidia kujenga ajira, kupunguza umaskini, upatikanaji wa masoko, kuwawezesha wanawake na kukuza ustawi wa makundi mengine katika mazingira magumu. Pia ni muhimu kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kupunguza hewa chafuzi wa hewa na kuboresha usalama barabarani.

Ametaja pia uhusiano wa usafiri na mabadiliko ya tabianchi akisema ni vyema kukabiliana na athari za mazingira zitokanazo na usafiri usio endelevu ili kuhakikisha kiwango cha joto hakizidi nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter