Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 10 kutoka Saudia kusaidia WFP Yemen

Dola milioni 10 kutoka Saudia kusaidia WFP Yemen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 10 kutoka Saudi Arabia kwa ajili ya kusaidia shirika hilo kukabiliana na utapiamlo huko Hodeidah nchini Yemen.

Makabidhiano ya msaada huo yamefanyika leo huko roma, Italia kati ya Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin na afisa Saudia Arabia Abdullah Al Rabeeah.

Msaada huo utaongezea juhudi za shirika hilo za kutoa mgao wa dharura wa chakula kwa karibu watu 465,000 kwa miezi sita nchini humo.

Bi Cousin akishukuru kituo hicho na Ufalme za Saudi Arabia amesema watu wengi nchini Yemen wanateseka kutokana na njaa kila siku ambapo kina mama hawana chaguo bali kuangalia watoto wao wakipungua uzito na kuangamia.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 14 kote nchini Yemen wanakumbwa na shida za kupata mahitaji yao ya chakula cha msingi ikiwemo milioni 7 ambao hawana uhakika wa chakula.