Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoa huduma za afya wawezeshwe kutambua ukatili dhidi ya wanawake-WHO

Watoa huduma za afya wawezeshwe kutambua ukatili dhidi ya wanawake-WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema wakati siku 16 za harakati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zimeanza zikienda sambamba na maadhimisho ya siku hiyo hii leo, watoa huduma za afya wathaminiwe kutokana na umuhimu wao.

WHO imesema kuwa kila siku watoa huduma za afya wana wajibu mkubwa wa afya za wanawake wanaofanyiwa ukatili.

Shirika hilo pia limesema kuwa takwimu zinaonyesha kwamba wanawake wengi wanaofanyiwa ukatili wana imani na wanaweza kueleza madhila hayo kwa kwa watoa huduma wa afya kwanza kabla ya kueleza kwa mtu mwingine.

Fadela Chaib ni msemaji wa WHO Geneva.

(SAUTI FADELA)

‘‘Mtoa huduma wa afya awezeshwe kutambua ishara za ukatili ili atoe huduma, usaidizi na ushauri ambao mwanamke anapaswa kupata.’’