Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wavukao Mediteranea mwaka huu yapungua

Idadi ya wavukao Mediteranea mwaka huu yapungua

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limesema idadi ya wahamiaji na wakimbizi wanaovuka bahari ya Mediteranea kusaka hifadhi Ulaya kuanzia Januari hadi mwezi huu wa  Novemba imepungua ikilinganishwa na mwaka jana.

Akizungumza na wanahabari huko Geneva, Uswisi, msemaji wa IOM Joe Milliman amesema idadi ya mwaka huu inakaribia Laki Tatu na Nusu ilhali mwaka jana katika kipindi kama hicho ilikuwa karibu Laki Tisa.

IOM I mesema wasaka hifadhi hao wanapitia Italia na Ugiriki, ingawa sababu ya idadi kupungua haikutajwa.

Shirika hilo limesema hata hivyo limeendelea kuokoa wahamiaji baharini huku wengine wakipoteza maisha.