Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwongozo wa FAO kusaidia ufugaji endelevu

Mwongozo wa FAO kusaidia ufugaji endelevu

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeandaa mwongozo wa kuboresha usimamizi wa maeneo ya ardhi yanayotumiwa na wafugaji. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

FAO inasema usaidizi kwa jamii za wafugaji ni muhimu siyo tu kwa kufanikisha lengo namba mbili la maendeleo endelevu, SDG la kutaka kutokomeza njaa na kuendeleza kilimo endelevu, bali pia lengo namba 15 la kutaka  uhifadhi wa aina zote za watu wanavyoishi bila kuharibu mazingira na bayonuai.

Kwa mantiki hiyo, mwongozo huo uliondaliwa na FAO na wadau wake ikiwemo kamisheni ya sheria za mazingira, unalenga kutoa uelewa wa masuala muhimu kuhusu ufugaji endelevu, kupata usimamizi na umiliki wa mbinu za kujipatia kipato bila kuharibu kanuni za kimila.

Shirika hilo limesema changamono ni kujumuisha pamoja mifumo ya kimila na ile ya kiserikali bila kupoteza mahitaji maalum ya wafugaji ambao wengine huhamahama kusaka malisho bora kwa mifugo yao.