Skip to main content

WHO na Sudan Kusini wafanikisha kampeni dhidi ya Polio

WHO na Sudan Kusini wafanikisha kampeni dhidi ya Polio

Nchini Sudan Kusini, shirika la afya duniani, WHO kwa kushirikiana na serikali wamefanikisha kampeni ya chanjo dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Polio kwenye jimbo la Unity.

Aina mbili za Polio zilibainika kwenye jimbo hilo mwezi Septemba 2014 na Aprili 2015 na kutishia ustawi wa watoto ambapo chanjo zilizotolewa kwa watoto zaidi ya 155,000 wenye umri wa chini ya miaka 15.

Vituo 15 vya utoaji chanjo viliandaliwa kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo hiyo katika nchi hiyo ambayo mzozo, kuhamahama na mafuriko vimekwamisha kampeni kufanyika kwa wakati.

Mwakilishi wa WHO nchini Sudan Kusini Dkt. Abdulmumini Usman amesema vituo hivyo 15 ni kati ya vituo 26 vya utoaji chanjo vilivyotengwa kwa ajili ya utoaji chanjo kwenye majimbo mbali mbali ili kuepusha mlipuko wa Polio.