Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama barabarani Afrika Mashariki

Usalama barabarani Afrika Mashariki

Tarehe 21 Novemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani. Katika kuadhimisha siku hiyo shirika la afya ulimwenguni WHO linasema vijana ndio wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kuliko watu wazima.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watu 3400 wanapoteza maisha barabarani kote duniani sawa na watu karibu milioni 1.3 kwa mwaka.

WHO ina lengo la kupunguza idadi hiyo kwa kuchagiza uboreshaji wa usalama barabarani. Je hali barani Afrika ikoje?