Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC yaweza kujijenga na kujibomoa-UM

DRC yaweza kujijenga na kujibomoa-UM

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ina fursa ya kujijenga au kijibomoa, pamoja na majirani zake amesema mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Mamadou Diallo

Takribani watu milioni nane wamethiriwa na mgogoro nchini humo.

Bwana Diallo amesema kuwa hali mashariki mwa taifa hilo imezuia ugawaji wa misaada, na kuongeza kuwa ukubwa wa nchi hiyo una umuhimu na hivyo mgogoro sio tu kuwa unaiathiri pekee bali pia majirani.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kati ya mwezi Julai na Septemba pekee ,watu 180,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mivutano ya wenyewe kwa wenyewe.