Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati Walibya wakikimbilia Ulaya, wengine wahamia nchini kwao: IOM

Wakati Walibya wakikimbilia Ulaya, wengine wahamia nchini kwao: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema leo kuwa, wakati maelfu ya raia wa Libya wakikimbia nchi yao kusaka hifadhi mataifa ya Ulaya, asilimia 81 hadi 83 ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika ikiwamo Misri, Chad na Sudan wananuia kuhamia Libya .

Taarifa ya IOM inasema hali ni tofauti kwa raia wa Nigeria ambao ni asilimia 16 tu wenye nia ya kusalia nchini humo wakati ambapo asilimia 43 ya raia hao wanakusudia kuendelea kusafiri kuelekea Italia.

Taarifa hiyo inasema kuwa asilimia 12 wananuia kwenda Ujerumani na asilimia iliyosalia katika mataifa mengine barani Ulaya.