Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunyonyesha watoto ni haki ya binadamu: UM

Kunyonyesha watoto ni haki ya binadamu: UM

Umoja wa Mataifa umesema kunyonyesha watoto ni suala la haki za binadamu kwa watoto na akina mama na linapaswa kulindwa na kupgiwa chepuo kwa faida ya wote.

Katika taarifa ya pamoja ya wataalamu huru wa UM, wameyataka mataifa kuchukua hatua za dharura kukomesha upotoshaji unofanywa na kampuni za kibiashara kuhusu unyonyeshaji mbadala usiozingatia misingi ya afya.

Wataalamu hao wamesema upotoshaji huo hufanywa na viwanda vya maziwa ambavyo huzalisha mabilioni kupitia ushawishi huo.

Kumekuwa na kampeni sehemu nyingi duniani kuhusu kunyonyesha watoto kwa maziwa yasiyo ya mama ambayo hujulikana zaidi kwa jina la maziwa ya kopo, ambayo inapigiwa upatu na kamopuni za biashara kwa lengo la kujinufaisha,.