Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maji waweza kuchochea mivutano-Ban

Ukosefu wa maji waweza kuchochea mivutano-Ban

Ifikapo mwaka 2050 takribani mtu mmoja kati ya wanne huenda akaishi katika nchi ambayo imeathirika na tatizo sugu la upungufu wa maji. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwenye mkutano wa ngazi ya juu Jumanne katika baraza la usalama ukijadili maji, amani na usalama. Amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yataongeza changamoto hususani katika mabonde ya kimataifa.

Ban amesema kuna haja ya uratibu katika usimamizi wa maji na hasa kwa mito zaidi ya 260 ya kimataifa na angalau kwa vyanzo vingi vya maji yanayotumika, kwa sababu.....

(SAUTI YA BAN)

Fursa ya kupata maji inaweza kuongeza mivutano ya kijamii, mashindano dhidi ya rasilimali kidogo ya maji Darfur na Afghanistan iyamechangia mivutano , Peru, athari za sekta ya madini katika maji ni chanzo cha kawaida cha maandamano na vurugu katika jamii dhidi ya makampuni.”

Amesema licha ya changamoto zote hizo ni lazima kutambua umuhimu wa ushirikiano katika matumizi na kuwekeza katika rasilimali ya maji ili kudumisha amani na usalama na sio migogoro.