Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Televisheni ni chombo mahususi kwa ajili ya taarifa kwa umma: UNESCO

Televisheni ni chombo mahususi kwa ajili ya taarifa kwa umma: UNESCO

04barazakuutvLeo ni siku ya kimataifa yaTelevisheni. Siku hii ilitangazwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka wa 1996 ili kuhamasisha kubadilishana vipindi vya televisheni kimataifa vikiangazia masuala ya amani, usalama, maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kubadilishana utamaduni.

Televisheni imekuwa moja y avyombo vya habari vyenye ushawishi mkubwa wakati huu ambapo UNESCO inasema inatambua umuhimu wa chombo hicho kama njia ya msingi ya mawasiliano kwa umma.

Televisheni kadhalika ina wajibu muhimu katika katika kusambaza taarifa na maarifa na hivyo hutumika kama taswira hali za binadamu na shauku zao imesema UNESCO.

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa televisheni ya umoja huo UNTV, imeandaa maonesho ya shughuli za chombo hicho na kutoa fursa kwa watu kuangalia utendaji wake.