Skip to main content

Mswada Bungeni Uturuki kuwapa msamaha wanyanyasaji wa watoto

Mswada Bungeni Uturuki kuwapa msamaha wanyanyasaji wa watoto

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la idadi ya watu UNFPA, kitengo kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women na lile la mpango wa maendeleo UNDP nchini Uturuki, wana wasiwasi na mswada wa mapendekezo utakaowasilishwa bungeni wakati wa mijadala ya kisheria iliyoanza tangu Novemba 17 ambayo inaweza kusababisha baadhi ya aina ya msamaha kwa unyanyasaji wa watoto kwa masharti kwamba wahusika watawoa wathirika.

Na ikiwa utapitishwa katika hali yake ya sasa, mswada huo utadhoofisha uwezo wa Uturuki wa kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na ndoa za utotoni, huku ukiwapa neema wahusika kwa ukiukwaji wa haki za watoto na kuongeza hatari zaidi ya mtoto kuolewa na mhusika.

Uturuki ni mwanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za mtoto na mkataba wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake.