Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko katika ngazi zote yanahitajika kwa kuleta usawa wa kijinsia kazini:UNDP

Mabadiliko katika ngazi zote yanahitajika kwa kuleta usawa wa kijinsia kazini:UNDP

Mabadiliko yanahitajika katika ngazi zote katika jamii ili kuboresha hali ya usawa wa kijinsia makazini , kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Wataalamu kutoka kila kona ya dunia wamekusanyika Panama Jumatatu kwenye kongamano la tatu la biashara kuhusu usawa wa kijinsia linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hilo litajikita katika jinsi gani sekta binafsi inaweza kuweka mazingira ya usawa na kujenga mazingira ya kazi jumuishi. Randi Davis, ni mkurugenzi wa timu ya masuala ya jinsia kwenye shirila la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Anaeleza masuala gani muhimu yanayowakabili wanawake kote duniani katika mazingira ya kazi

(SAUTI YA RADI DAVIS) 

“Wanawake kote duniani wanaendelea kulipwa asilimia 24 chini ya wanaume na wengi wako katika madaraja ya chini, hivyo moja ya mambo muhimu ya kazi yetu ni kuwasukuma wanawake wafikie katika ngazi za maamuzi makazini. Tunataka kuwaona wanawake kote duniani ambao wanasoma kama wanaume au zaidi na hatuwaoni kwenye ngazi za juu wanafika huo, tunajitaji kufanya mabadiliko katika ngazzi zote, tunahitaji sera ya umma ambayo inawawezesha wanawake kuendelea katika ujuzi wao, pia tunahitaji mabadiliko katika tabia za unaguzi wa kijinsia makaziniili kuhakikisha wanawake wanapiga hatua  kwa mazingira ya kazi.”