Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvuvi unaingiza dola bilioni 135 kila mwaka:FAO

Uvuvi unaingiza dola bilioni 135 kila mwaka:FAO

Sekta ya uvuvi kimataifa inaingiza wastani wa dola bilioni 135 kwa mwaka kama mapato ya usafirishaji nje wa vidhaa zake, limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Sekta hiyo pia inatoa ajira au kipato kwa mtu mmoja kati ya 10 duniani huku pia ikiwa chanzo kikubwa cha asilimia 17 ya vyakula vya kujenga mwili au ptotini vinavyoliwa kote duniani.

Akizungumza katika mkutano maalumu ulioandaliwa na FAO na Holy kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na uvuvi haramu katika sekta ya uvuvi, mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema sekta za uvuvi

(SAUTI YA GRAZIANO-CUT 1)

“zinatoa ajira , zinajenga sekta imara za mwambao na zinatoa lishe na uhakika wa chakulakwa watu wasiojiweza. Bidhaa za uvuvi miongoni mwa bidaa zinazouzwa sana duniani. Samaki hivi sasa zinaingiza pato kubwa kwa nchi zinazoendelea kuliko mchele, tumbaku , nyama na sulari kwa pamoja.

Hata hivyo amesema kila kitu sio mana na asali katika sekta hiyo

(GRAZIANO-CUT 2)

“Chakusikitisha sekta hiyohiyo inayotoa fursa nyingi ndiyo pia inayowaathiri watu wasiojiweza, shirika la kazi duniani ILO linakadiria kwamba kila mwaka wavuvi wanawake na wanaume 24,000 wanapoteza maisha yao.Pia tunashuhudia duru za habari za ukkiukwaji wa haki za binadamu katika sekta hii, kote nchi zilizoendelea na zinazoendelea vikijumuia ukatili makazini, ajira za lazima, usafirishaji haramu , ajira kwa watoto na utumwa.”

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uvuvi FAO na Holy See wanatoa wito wa ushirikiano na wadau wote kufanya kazi pamoja ili kutokomeza ukiukwaji huo wa haki za binadamu na kuhakikisha ajira zenye hadhi kwenye sekta ya uvuvi.