Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna tena hospitali Allepo, UM wasikitishwa.

Hakuna tena hospitali Allepo, UM wasikitishwa.

Mji wa Allepo nchini Syria sasa hauan hospitali baada ya kufungwa kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni, limesema shirika la afya ulimwenguni WHO.

Hali katika mji huo hususani mashariki imezidi kuwa mbaya tangu mwezi Julai mwaka huu ambapo wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu walipata fursa ya mwisho kuwafikiwa watu zaidi ya 250,000 katika eneo hilo lilolozingirwa.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Staffan de Mistura amesema amesikitishwa na taarifa za kupigwa mabomu kwa hospitali mjiniAllepo, wakati alipokutana na wawakilishi wa serikali mjini Damascus.

Amesema kadhalika watoto wanaendelea kuuliwa na mfululizo wa mabomu yanayoporomoshwa magharibi mwa Allepo na kwamba hakukuwa na makubalinao yaliyofikiwa dhidi ya serijkali kuhusu kuruhusu watoa misaada wa UM kuyafiia