Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 3400 hupoteza maisha kila siku kwa ajali za barabarani:

Zaidi ya watu 3400 hupoteza maisha kila siku kwa ajali za barabarani:

Vijana ndio wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kuliko watu wazima limesema shirika la afya ulimwenguni WHO.

Katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kila siku watu zaidi ya 3400 wanapoteza maisha barabarani kote duniani sawa na watu karibu milioni 1.3 kwa mwaka.

WHO ina lengo la kupunguza idadi hiyo kwa kuchagiza uboreshaji wa usalama barabarani. Wazazi wa binti aliyepoteza maisha baada ya kugongwa na gari mjini New York wanazungumzia juhudi wanazozifanya kuhakikisha wazazi wengine hawapitii machungu waliopitia

(SAUTI YA WAZAZI)

Mama:Alikuwa mchangamfu nab inti mwenye furaha, alikuwa anaingia ndani ya basi namba 44 na kuimba wheels of the bus go round and round,

Baba:watu wa New York kila wakati wanaharaka, lakini tunawapa changamoto madereva kutulia kidogo nakujiuliza je inastahili? Je inastahili kumgonga mtoto eti kwa sababu umechelewa? Je inastahili kuongea na simu wakati inamaanisha kuna familia inampeleka kaburini mtoto wao?je inastahili kumtumia ujumbe wa simu rafiki yao wakati ukijua baba ananukuu muda huo kwa kuandaa mazishi ya mwanae?