Mkutano kuhusu anga na maendeleo waanza Dubai

21 Novemba 2016

Wanaanga, wakuu wa mashirika ya anga na wawakilshi wa jumuiya ya kimataifa ya anga wanakutana Dubai juma hili kujadili namna ya kutoa usaidizi kwa maendeleo kimataifa.

Mkutano huu wa ngazi ya juu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa na Falme za Kiarabu umendaliwa na ofisi ya UM kuhusu masuala ya anga UNOOSA na shirika la masuala ya anga la Falme za Kiarabu

Mkutano huu unakuja wakati huu ambapo sekta ya anga inakua, huku wadau wakiongezeka. Majadiliano yatajikita zaidi katika anga uchumi, anga jamii, upatikanaji wa anga na anga diplomasia.

Akizungumza kuhusu mkutano huo Mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya anga Simonetta Di Pippo amesema mkutano  huu wa kwanza ni mwanzo mzuri katika mchakato wa kuanzisha ushirikiano na uratibu wa jamii , na kupanua kwa watumiaji wengine wa jamii, kwa lengo mahsusi la sekta ya anga kwa uchumi,jamii na maendeleo ya mataifa yote.’

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter