Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwanda endelevu ndio mwarubaini wa kukua kwa uchumi Afrika: Ban

Viwanda endelevu ndio mwarubaini wa kukua kwa uchumi Afrika: Ban

Kongeza uzalishaji na viwanda ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo endelevu Afrika amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Katika ujumbe wake wa kudhimisha siki hiyo hii leoNovemba 20, Ban amesema ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu katika lengo namba tisa linazungumzia ugunduzi na miundombinu kwani tafiti zinaonyesha kuwa viwanda sio tu vinazalisha ajira,  bali ajira maradufu.

Amesema wakati bara Afrika likiadhimisha siku hii, Umoja wa Mataifa unatoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia fedha kwa ajili ya viwanda endelevu na jumuishi. Ban ameongeza kuwa ili kutimiza hili mataifa barani Afrika yanahitaji sera zitakazohamasiha ukuaji wa sekta binafsi, kuwezesha juhudi za ujasiriamali, kuongeza uwekezaji na kukuza ubia.

Katibu Mkuu amesema kwa muongo mmoja uliopita maendeleo Afrika yamekua kwa asiliamia 4.7, na licha ya kasi hiyo kupungua mwaka jana , lakini bara hilo  linasalia  kuwa ukanda unaokuwa kwa kasi zaidi dunaiani.