Vyoo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi

Vyoo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi

sikuyavyooLeo ni siku ya choo duiani, Umoja wa Mataifa unasema siku hii ni muhimu kwa ajili ya kuhamasisha hatua za upuuzwaji wa huduma za kujisafi ambazo hazipewi kipaumbele na kukuza uchumi.

Maudhui ya mwaka huu ni vyoo na ajira na umuhimu wa huduma za kujisafi au ukosefu wake katika ustawi na mazingira ya kazi.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema vyoo vina mchango muhimu katika kujenga uchumi imara, na ukosefu wa vyoo maeneo ya kazi na nyumbani una madhara makubwa kupunguza uzalishaji.

Kwa mujibu wa takwimu za UM karibu asilimia 17 za vifo makazini zinasababishwa na magonja ya kuambukiza .

Takwimu pia zinaonyesha kuwa upatiakanaji wa huduma za maji na kujisafi  (kunawa), zaweza kukuza uchumi, wakati ambapo kiasi cha dola bilioni 260 zinapotea kila mwaka kwa kukosa huduma za usafi na maji salama.