Mali yatakiwa kuhakikisha amani wakati wa uchaguzi

Mali yatakiwa kuhakikisha amani wakati wa uchaguzi

maliuchaguziUmoja wa Mataifa umeitaka Mali kujiepusha na vurugu zinazoweza kujitokeza kabla na baada ya uchaguzi wa manispaa mnamo Novemba 20 mwaka huu, uchuguzi ambao umeahirishwa mara tatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon imemkariri akionya kuwa  hali ya kiusalama kaskazini na baadhi ya maeneo ya kati mwa nchi yanaweza kuvuruga utaratibu wa uchaguzi.

Ameitaka serikali kuwezesha majadiliano ya kujenga  na wadau wote kabla na baada ya kura ili kutovuruga mkataba wa awali wa amani.

Mapigano katia ya vikosi vya serikali na waasi wa Tuareg yamesababisha ukosefu wa utulivu katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.