Skip to main content

Mapigano kusitishwa kwa saa 48 Yemen.

Mapigano kusitishwa kwa saa 48 Yemen.

yemenmisaada Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa pande kinzani nchini Yemen zimakubali kusitisha mapigano kwa muda wa kuanzia wa saa 48.

Tangu mwaka 2014, mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Houthi vimesababisha vifo vya takribani watu 10,000.

Kwa mujibu wa tarifa ya mjumbe maalum wa umoja huo nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, usitishaji wa mapigano unatarajiwa kuanza saa sita usiku kwa saa za Yemen.

Usitishwaji huo wa mapigano ni muhimu ili kuepuka umwagaji damu zaidi na uharibifu pamoja na kuruhusu ufikishwaji wa misada ya kibinadamu amesema Ahmed katika tarifa yake.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa watu wa Wayemen milioni 28 wana uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu.