Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokuwepo usawa wa kijinsia kwaigharimu Afrika mabilioni ya dola:UNDP

Kutokuwepo usawa wa kijinsia kwaigharimu Afrika mabilioni ya dola:UNDP

Kutokuwepo usawa wa kijinsia kunaligharamu bara la Afrika wastani dola bilioni 95 kila mwaka na kupanda hadi kufikia dola bilioni 105 mwaka wa 2014 au asilimia sita ya pato la ndani la taifa wa kanda hiyo.

Hii inahatarisha juhudi za bara hilo katika masuala ya maendeleo ya binadamu na ukuaji wa uchumi imesema ripoti ya 2016 ya maendeleo ya binadamu barani Afrika iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP. Ofisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) nchini Tanzania ikishirikiana na Ofisi ya Shirika la UNDP nchini humo wamezindua ripoti hiyo leo Jumatatu.

Ripoti hiyo ina uchambuzi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii na mambo yanayodhoofisha maendeleo ya wanawake barani Afrika. Inapendekeza sera na hatua madhubuti kuziba pengo hilo zikijumuisha kushughulikia vifungu vya sheria za jinsia; kanuni zinazoleta madhara kwenye jamii na kubadilisha mazingira ya kibaguzi katika taasisi na wanawake kupata ushiriki kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Akihojiwa na idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, Dr Rodgers Dhliwayo, mshauri wa uchumi wa UNDP nchini Tanzania anasema..

(Sauti ya Dr. Dhliwayo)

Kuna nchi ambazo vimefanya vyema sana kisiasa kama vile Rwanda lakini kuna nchi nyingi bado zina changamoto.

Na kama mnavyofahamu usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake ni moja ya mambo yatakayoleta maendeleo endelevu.