Madhila ya ugonjwa wa kisukari na tiba yake

Madhila ya ugonjwa wa kisukari na tiba yake

Jumamatu Novemba 14 wiki hii, dunia imeadhimisha siku ya kisukari.   Shirika la afya ulimwenguni WHO ni kiranja katika mapambano dhidi ya gonjwa Hilo hatari.

Katika ujumbe wake kwa siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni muhimu kujikita katika kinga na kuimarisha huduma za afya. Ban amesema ugonjwa wa kisukari unaongoza katika kusababisha uono hafifu na upofu kwakuwa mabadiliko hayo yahana maumivu na ni ya taratibu na hivyo watu hugundua tatizo pale uono wao unapotatizika.

WHO kwa upande wake imesisitiza kuwa gonjwa hili linahitaji kuchukuliwa hatau zaidi kwani linaongezeka. Mathalani katiak takwikmu zake WHO inasema tangu mwaka 1980 kiwango cha wagonjwa kimeongezeka mara mabili

Shirika hilo limeongeza kuwa zaidi ya watu wazima milioni 400 wameugua kisukari mwaka 2014 .Miongoni mwao karibu milioni moja na nusu hufa kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret chan katika ujumbe maalumu anataja hatua za tiba dhidi ya kisukari.

( SAUTI MARGARET)

"Hatua ya awali  ili kuishi vyema na kisukari ni tiba mapema, kisukari chaweza kutibiwa, na gonjwa hili laweza kudhitiwa kwa  njia mbili, kubadili mfumo wa maisha na dawa muafaka ikiwamo zile ambazo zaweza kushusha shinikizo la damu na kiwango cha lehemu.  Mara nyingi dawa muhimu na teknolojia za tiba ya kisukari na udhibiti wake havipatikani katika jamii na nchi masikini"

Tuangazie sasa hali katika nchi zenye kipato cha chini. Tuelekee Tanzania. kwake Anatory Tarimo  wa redio washirika Karagwe Fm ya Kagera.