Baraza la usalama lajadili ushirikiano kati ya UM na AU

18 Novemba 2016

barazaauBaraza la usalama leo limekuwa na majadala kuhusu kukuza ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muugano wa Afrika, AU katika kukuza amani na usalama.

Akihutubia baraza hilo, msaidizi wa Katibu Mkuub wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Haile Menkerios amesema mchango wa Afrika kwa umoja huo ni bayana akitolea mfano wa vikosi vyau linzi wa amani kutoka barani humo.

Amesema katika kutatua changanoto za amani na usalama duniani ushirikiano huo haukwepeki.

( SAUTI HAILE)

‘Wakati Umoja wa Mataifa una jukumu la msingi la kukuza amani na usalama, Muungano wa Afrika ni moja ya wadau wetu muhimu katika kuzikabili changamoto za pamoja Afrika.’’

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter