Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki: Tashwishi na Tafrani

Neno la wiki: Tashwishi na Tafrani

Katika neno la wiki tunachambua maneno Tashwishi na Tafrani , mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Maswala ya Mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Tashwishi na Tafrani ni maneno mawili tofouti, hayana uhusiano wowote. Tafrani ina maana mbili, mosi ni msumbuko wa moyo au shauku, ni kutokuwa na uhakika na jambo fulani. Pili, katika maswala ya kisiasa tafrani ni vile mambo inavyokwenda visivyo au kuwa na vurugu, si ugomvi wa kupigana bali ni mambo yanakwenda usivyotaka.

Tashwishi ni kuwa na shuku au kutokuwa na uhakika wa jambo fulani.