Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani itashirikiana na UM chini ya utawala wa Trump:Eliasson

Marekani itashirikiana na UM chini ya utawala wa Trump:Eliasson

[caption id="attachment_300433" align="aligncenter" width="615"]dailynews230d-16

Uchaguzi wa Donald Trump kama Rais wa Marekani hautobadili ushirika wa muda mrefu baina ya Marekani na Umoja wa Mataifa. Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSEMARY)

Ujumbe huo umetolewa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, alipozungumza na waandishi wa habari Ijumaa mjini Geneva Uswis.

Amesema amekutana na Rais huyo mteule Trump mara mbili siku za nyuma na hajashuhudia mtazamo wowote wa uadui dhidi ya Umoja wa mataifa

(SAUTI YA ELIASSON)

"Hivyo nguzo yetu katika kufanya kazi ni kwamba Marekani itaendelea kufanya kazi na Umoja wa Mataifa, si tu kwa sababu yangu, bali ni jambo sahihi kufanya, lakini pia, ni katika maslahi binafsi ya nchi ypyote Wanachama, hasa mataifa makubwa.”

Bwana Eliasson ameelezea mchango mkubwa wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa ,ikiwemo katika ulinzi wa amani, kuchukua hatua katika masuala ya kibinadamu, kupigania haki za binadamu na utawala wa sheria.