Skip to main content

Pazia la COP 22 likifungwa EU yasema kuna matumaini ya utekelezaji

Pazia la COP 22 likifungwa EU yasema kuna matumaini ya utekelezaji

Pazia la mkutano wa 22 nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko wa tabia nchi COP 22 limefungwa leo mjini Marrakech Morocco, ambapo mada kadhaa zikiwamo usaidizi kwa Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uhakika wa chakula na nafasi ya jinsia na vijana zimejadiliwa. Patrick Newman na taarifa kamili.

( TAARIFA YA PATRICK)

Wawakilishi wa nchi na taasisi mbalimbali wameelezea matumaini yao katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kulingana na mkataba wa Paris.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mjini Marrakech, Kamishna wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na nishati katika kamisheni ya Umoja wa Ulaya EU Miguel Arias Cañete anasema utashi wa washiriki wa mkutano utasukuma utekelezaji.

( SAUTI MIGUEL)

‘‘Kuna utashi wa kutosha, sio tu kwa nchi, pia asasi za kiraia, wafanyabiashara pia wapo hapa, wamepanga na wana misingi.  Kwa hiyo ni suala mtambuka kwa wadau wote, wa umma na binafsi.’’