Tushikamane na ishara ndogo ya matumaini Sudan Kusini: Løj.

18 Novemba 2016

Ni lazima kusalia katika ishara ndogo ya matumaini, amesema Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nhini Sudan Kusini na mkuu wa ujumbe wa umoja huo nchini humo UNMISS Ellen Margarethe Løj.

Katika mahojiano maaulum na redio ya Umoja wa Mataifa na idhaa hii, kiongozi huyo anayemaliza muda wake wa uongozi, amesema hali ya kibinadamu ni mbaya lakini alipoulizwa kama kuna dalili yoyote ya matumaini akasema.

( SAUTI LOJ)

‘‘Huwezi kuwa mkuu wa ujumbe wa kulinda amani nchiniSudan Kusini na usishikamane na ishara ndogo ya matumaini. Inaonekana ngumu sana, na ni ngumu hakika. Hatuwezi kukata tamaa, kwasababu tukikata tamaa, ni watu wa Sudan Kusini ambao wanateseka.’’

Bi Løj hapo jana amelihutubia baraza la usalama ambapo pia amesema viongozi wa tiafa hilo wanapaswa kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kutekeleza mkataba wa makubaliano ya amani

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter