Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya watoto njiti duniani:WHO/PAHO

Leo ni siku ya watoto njiti duniani:WHO/PAHO

Leo ni siku ya kimataifa ya watoto njiti, siku ambayo ilianzishwa kwa nia ya kuelimisha kuhusu kujifungua watoto njiti ambao hawajakomaa na fikisha wiki 37.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la mataifa ya Amerika PAHO, tatizo la watoto njiti ni chanzo kikubwa cha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Katika kuadhimisha siku hii iliyoanza kuadhimishwa mwaka 2011, PAHO leo Alhamisi imefanya mkutano kuhusu kuzuia upofu unaosababishwa na hali ya kuzaliwa njiti , ugonjwa onaoongoza kwa watoto njiti  na ambao unazuilika na kutibika.