WHO yakaribisha ufadhili wa chanjo:

17 Novemba 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na chanjo wa shirika la afya dunia WHO, Dk Jean-Marie Okwo-Bele leo amekaribisha na kupongeza mashirika yote yaliyohusika kufanikisha ufhadili wa shirikika hilo kupitia mipango ya chanjo.

Katika ufadhili huo mfuko wa kimataifa wa Kupambana na ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (global Fund), leo limepitisha  dola za kimarekani milioni 15 kwaajili ya chanjo ya malaria, ikiwa ni fedha kamili kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mpango huo.

Mapema mwaka huu, Shirikia la chanjo la kimataifa Gavi na UNITAID walitangaza ahadi ya dola milioni 27 na kisha milioni 9.6, kwa kipindi cha miaka minne ya mpango wa chanjo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter