Afrika kufaidika kwanza na mfumo wa tahadhari ya majanga:COP22

Afrika kufaidika kwanza na mfumo wa tahadhari ya majanga:COP22

Nchi za Afrika zenye maendeleo dunia na visiwa vya Pacific watakuwa wa kwanza kufaidika na mfumo ulioboreshwa wa tahadhari dhidi ya hali ya hewa na athari zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia mkakati wa kuchukua hatua ulioainishwa na mkutano wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea Morocco.

Nchi hizo zikiwemo Mali, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC nan chi za visiwa vidogo zinazoendelea , zitapatiwa msaada wa awali wa dola milioni 12 zilizotengwa na mradi wa athari za mabadiliko ya tabia nchi na tahadhari ya mapema (CREWS).

Mradi wa CREWS ulizinduliwa 2015 wakati wa mkutano wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi na lengo lake ni kukusanya dola milioni 30 ifikapo Julai 2017 na dola milioni 100 ifikapo 2020 kukabili mabadiliko ya tabia nchi.