Mafunzo yabadili maisha ya wakulima nchini Kenya

Mafunzo yabadili maisha ya wakulima nchini Kenya

Wakati athari za mabadiliko ya tabianchi zikishuhudiwa wakulima wanaenedeleza shughuli za kilimo chenye tija kama njia moja ya kukabiliana na athari hizo. Nchini Kenya wakulima wanalima mashamba ambayo yanazalisha mazao na kuleta kipato cha juu sanjari na chakula chenye virutubisho hii ikiashiria uwezekano wa kilimo chenye tija kama mbinu ya kustahimili mabadiliko ya tabianchi.

Katika makala hii Grace Kaneiya anatupeleka katika kijiji kilichoko Nyando nchini Kenya ambako tunakutana na mkulima Joshua, ambaye anasema mafunzo ya kilimo hai na ufugaji wa kisasa yamemsaidia kuimarisha shamba lake.