Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Falsafa ni kuishi kwa utu: UNESCO

Falsafa ni kuishi kwa utu: UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya falsafa duniani, katika kuadhimisha siku hii, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na teklnolojia UNESCO, linaandaa matukio mbalimbali hadi Novemba 19, ili kusherehekea ubunifu na nidhamu katika utofauti miongoni mwa watu.

Taarifa ya UNESCO inasema umuhimu wa siku hii unatokana na ukweli kwamba inaadhimishwa siku moja baada ya siku ya kimataifa ya stahamala, kwani dhana hizo mbili zina mahusiano kwani falsafa inajikita katika maelewano, heshima na kujali utofauti wa maoni kuhusu utamaduni wa namna watu wanaovyoishi.

Falsafa inaelezwa kuwa ni sanaa ya kuishi kwa kuzingatia haki na maadili ya pamoja ambayo ni misingi ya stahamala, imefafanua taarifa hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amenukuliwa akisema falsafa ni zaidi ya somo la drasani, ni maisha ya kila siku, yanayowasaidia watu waishi katika namna ya utu zaidi.