Skip to main content

Licha ya changamoto Somalia imepiga hatua:Buik

Licha ya changamoto Somalia imepiga hatua:Buik

Christoph Buik, Kamishna wa Polisi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, akihojiwa na radio ya Umoja wa Mataifa, amesema kuna maendeleo makubwa nchini humo ingawa ni ya pole pole kutoka na usalama ambao bado ni tete na tishio la kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.

Bwana Buik ameyasifu majeshi ya Muungano wa Afrika nchini humo AMISON na jeshi la kitaifa kwa kuendelea kupambana na kikundi hicho. Kuhusu uchaguzi nchini humo ambao ni wa kwanza wa kidemokrasia kwa miaka 47, amesema unaendelea vyema kama nchi inavyoendelea kupata nafuu kutokana na migogoro mbali mbali ya kiraia na athari za ukame.

Na kuhusu kazi ya polisi wa Umoja wa Mataifa nchini humo amesema…

(Sauti ya Buik)

Sisi kama polisi tunajari bu kuwezesha mamlaka kuwa na uwezo wa kujihimili. Kwa muda wa miaka minne iliyopita Somalia imepinga hatua kubwa kimaendeleo, serikali ikishika usukani na mamlaka zingine wanajitahidi, itawachukua muda mrefu lakini wanaendelea vyema