Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika imenifurahisha katika hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi:Ban

Afrika imenifurahisha katika hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi:Ban

[caption id="attachment_301456" align="aligncenter" width="615"]dailynews229a-16

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ameridhishwa na hamasa ya nchi za Afrika katika kuchukua hatua kukabili mabadiliko ya tabia nchi.  Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Akizungumza kwenye kikao cha ngazi ya juu cha hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi mjini Marakech Morocco, Ban amesema , Morocco, nchi nyingine zaidi ya 30 za Afrika taasisi kubwa za maendeleo wamekusanya nguvu ili kuchagiza miradi ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa Afrika.

Amesema ushirika huo utasaidia kuweka mifumo imara zaidi ya chakula inayohimili mabadiliko katika bara la Afrika na kupiga hatua katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s.

Amezichagiza pia sekta zote katika jamii kushiriki mchakato huo kwani mchango wa kila mtu na katika ngazi zote unahitajika.

Na kuhusu utekelezaji wa mkataba wa Paris ameongeza

(SAUTI YA BAN)

“Sasa wakati mkataba wa Paris umeanza kutekelezwa , kila mtu ana matarajio, inabidi tuutekeleze kwa vitendo mashinani. Kila hatua ni muhimu katika juhudi zetu”