Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nigeria toeni maelezo kwanini kuwafukuza watu 30,000: UM

Nigeria toeni maelezo kwanini kuwafukuza watu 30,000: UM

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za makazi Leilani Farha ameitaka serikali ya Nigeria kutoa maelezeo haraka juu ya watu 30,000 waliofukuzwa jimboni Lagos juma lililopita.

Taarifa ya mtaalamu huyo inasema hatua hiyo imefanyika kwa kile kilichoitwa operesheni ya maendeleo ya kusafisha maeneo yaliyopakana na maji.

Watu wanne wanaripotiwa kufa katika operesheni hiyo ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, watu waliothirika wanatoka eneo liitwalo Eugun na wengine kutoka makabila yenye idadi ndogo ya watu na ambao wana kipato kidogo na waliishi katika maeneo duni kaibu na maji.