Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabilioni ya dola yahitajika kuinusuru CAR:

Mabilioni ya dola yahitajika kuinusuru CAR:

Dola takribani bilioni tatu zinahitajika ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kujikwamua baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokatiki maelfu ya watu na kuliacha taifa hilo njia pandakiuchumi, kiusalama na kimaendeleo. Hayo ni kwa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson anayehudhuria mkutano maalumu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya CAR mjini Brussel Ubelgiji. Mkutano huo unajumuisha wahisani kutoka nchi za Muungano wa Ulaya, Bank ya Dunia na Umoja wa Mataifa. Eliasson ameongeza

(ELIASSON CUT)

"Huu mkataba wa leo utasaidia nchi kwa kisiasa ,kuleta amani na kutoa mwelekeo wa muafaka, maridhiano na maendeleo. Leo, zaidi ya siku zote , watu wake wanahitaji ahadi ya muda mrefu na msaada"

(SAUTI YA TOUADERA)

"Sisi kama wananchi lazima tubadilishe mawazo yetu na tusijikandamize ambayo imekuwa kama historia, ni lazima tupinge mauaji na tutimize wajibu wakujiinua , tuondoe tofauti kati yetu na tuinuie nchi yetu"