Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upokonyaji silaha na ujumuishwaji ni muhimu katika kupunguza machafuko: Titov

Upokonyaji silaha na ujumuishwaji ni muhimu katika kupunguza machafuko: Titov

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kupunguza machafuko katika jamii na dhana ya ulinzi na ujenzi wa amani mapema umeanza hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mjadala huo unakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya mpango wa kupunguza machafuko katika jamii ambapo washiriki wa mkutano huo ambao ni wadau wa masuala ya amani na ulinzi wake wamesema bado kuna mengi ya kufanya katika kutimiza lengo la mpango huo.

Akizungumzia umuhimu wa upokonywaji wa silaha, na ujumuishwaji kwenye jamii DDR, katika kupunguza machafuko, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu taasisi za utawala wa sheria na usalama katika ulinzi wa amani DPKO Dmitry Titov amesema .

( SAUTI DMITRY)

‘‘Tunatambua umuhimu wa DDR katika kupunguza machafuko kwenye jamii,na katika ripoti ya Katibu Mkuu tuna kipengele maalum, na tunatarajia mkutano maalum kuhusu hilo kabla ya mwisho wa mwaka.’’