Sudan Kusini inaangamia kwa kasi-Ging

16 Novemba 2016

Mkuu wa Operesheni za Kibinadamu katika Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibidamu, OCHA, John Ging amesema hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini inaendelea kuwa mbaya ikichangiwa na ukosefu wa usalama.

Akizungumza nawanadishi wa habari kuhusu ziara yake katika nchi tatu ambazo zinasaidiwa na jujuiya ya kimataifa kutokana na majanga ya asili na ya kibinadamu ambazo ni Haiti, Sudan na Sudan Kusini, amesema ni wazi kuwa nchi hiyo yaweza kutumbukia katika mauaji ya kimbari.

Amesema mifumo muhimu kama elimu na huduma nyingine za kijamii imesambaratika Sudan Kusini kwa asilimia kubwa lakini kipo kinamchomtia moyo kwa watu wa taifa hilo changa duniani.

( SAUTI GING)

‘‘Utu na ujasiri walionao unatia moyo, hasa kuona jinsi watu walivyo na tumaini, lakini tusiache kutambua kuwa ni hali ambayo inadorora kwa kasi na watu wameteseka.’’

Akizungumzia ziara yajke nchini Haiti mkuu huyo wa opersheni za kibinadamu katiak UM amesem bado usaidizi wa kibinadamu unahitajika hasa kwa kuchukulia kwamba changizo lililotolewa halitoshi na mahitaji ni makubwa.

Kuhusu Sudan Ging amesema watu karibu milioni sita wanahitaji msaada wa kibinadamu na kuitaka jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter