Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadili ya kustahmiliana yakabiliwa na mtihani mkubwa- Ban

Maadili ya kustahmiliana yakabiliwa na mtihani mkubwa- Ban

Maadili ya stahmala na maelewano ya pamoja ambayo yamo ndani ya katiba ya Umoja wa Mataifa hivi sasa yanakabiliwa na mtihani mkubwa.

Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku ya stahmala duniani hii leo.

Amesema ukosefu wa kustahmiliana na kuvumiliana umesababisha watu kukimbia makwao na kusaka hifadhi ugenini, ambako nako mustakkhbali wao uko mashakani.

Ametaja pia watu kulengwa kwa sababu za imani zao za kidini, rangi zao bila kusahau makabila.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unapigia chepuo stahmala kama msingi wa utambulisho wake akisema kustahimiliana kunapozingatiwa ni mifano ya kuigwa na kunapotishiwa, ni lazima chombo hicho kipaze sauti.

Kwa mantiki hiyo ameseka katika siku hii, kila mtu apazei sauti ya umoja kwa mujibu wa kampeni ya Umoja wa Mataifa na fikra ya sisi na wao ichukuliwe na ile ya sisi wamoja.