Skip to main content

Chanda chema huvishwa pete, Mwelu kutoka Kenya ni mshindi wa tuzo,UNFCU

Chanda chema huvishwa pete, Mwelu kutoka Kenya ni mshindi wa tuzo,UNFCU

Shirikisho la mikopo la Umoja wa Mataifa, UNFCU , limetoa tuzo kwa washindi wa shindalo la picha kwa mwaka 2016. Tuzo hizo hujumuisha washiriki wa jumuiya ya Umoja wa Mataifa kutoka kila pembe ya dunia. Wanachotakiwa kufanya ni kuwasilisha picha za ubunifu zinazoelezea malengo ya maendeleo endelevu au SDGs binafsi, wafanyapo kazi na wanakoishi.

Mamia walijitokeza na kuwasilisha picha zao, lakini mwisho wa siku washiriki watatu ndio waliotunukiwa tuzo. Mpiga picha za sinema kutoka Jamaica Ryan Eccleston ndiye aliyeshikilia nafasi ya tatu. Mshindi wa pili ni Sristi Pradhan kutoka Nepal anayesoma Chuo Kikuu cha New York hapa Marekani na aliyeshika nafasi ya kwanza ni Julius Mwelu Manyasi kutoka Kenya. Amezungumza na Flora Nducha kuhusu shindano hilo na picha yake iliyoshinda

(MAHOJIANO MWELU)