Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara mtandaoni kukuza soko Afrika-UNCTAD

Biashara mtandaoni kukuza soko Afrika-UNCTAD

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa kupitia kituo cha kimataifa cha biashara ITC, imesema bishara mtandoni inatarajia kunufaisha nchi zinazoendelea hususani Afrika Mashariki.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Olivier Naray ambaye ni afisa progarmu wa UNCTAD amesema mpango huo umechagua nchi na sekta maalum ambapo Kenya na Uganda zimechaguliwa katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano hususani biashara mitandaoni.

Amesema kile ambacho wanakitarajia.

(SAUTI OLIVIER)

‘‘Baada ya takribani miaka minne ya mpango huu, tunatarajia matokeo mazuri kwani wamefunzwa kuhusu mauzo , namna ya kuimarisha ukurasa wako wa manunuzi, kujitangaza na kuimarisha nembo yako.”

Mpango huo ambao unafadhiliwa kwa pamoja na UNCTAD na Uholanzi unatarajia kuongeza ushindani katika kusafirisha bidhaa na kupata soko.